ZANZIBAR-Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuwasaidia watoto na wazee wenye mahitaji maalum katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mariam Mwinyi amesema hayo alipovitembelea Vituo vya kuwalea Watoto SOS, Mazizini na cha Wazee Welezo kuwapa msaada wa vyakula, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 5 Machi 2025.
Aidha, Mariam Mwinyi ameeleza kuwa ataendelea kuwasaidia zaidi watoto na wazee wenye mahitaji maalum ikiwemo vyakula katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Sikukuu ya Eid.
Mariam Mwinyi amewahimiza watoto kuwa wenye tabia njema na kufanya ibada katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani .
Halikadhalika Mama Mariam Mwinyi amewasilisha salamu za upendo kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika vituo hivyo.
Tags
Dkt.Hussein Ali Mwinyi
Habari
Mama Mariam Mwinyi
Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF)
Zanzibar News