Mashindano ya Quran ni ishara ya uhuru wa kuabudu-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quraan ni kielelezo thabiti cha kuwepo kwa uhuru wa kuabudu hapa nchini.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza katika Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Mabara yote katika Kuhifadhi Quraan yalioandaliwa na Taasisi ya Al-Hikma Foundation yàliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewasihi wazazi kuwahimiza watoto wao Kuhifadhi Quran ili kuongeza Masheikh na Maulamaa wa baadae.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuisoma na kuhifadhi Quran Tukufu, hasa katika Mwezi huu wa Ramadhani, huku wakitubu na kusaidia jamii wenye uhitaji.

Aliyeibuka mshindi wa mashindano hayo ni Aimeddin Farkhudinov kutoka Urusi; nafasi ya pili imeshikwa na Abdulmuhaimin Jumah kutoka Libya, mshindi wa tatu akawa Eslam Ahmed kutoka Misri.
Washiriki wengine walioshiriki wametokea nchi mbalimbali duniani zikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Ivory Coast, Nigeria , Burundi , Rwanda, Namibia, Morocco, Australia, Uingereza na Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news