PWANI-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejidhatiti katika kuboresha maisha ya walimu nchini, hususan katika maeneo ya maslahi na mazingira ya kazi.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Rufiji, mara baada ya walimu hao kufanya uchaguzi wa viongozi katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Ikwiriri.

Aidha, Waziri Mchengerwa amebainisha kuwa Taifa lina bahati ya kuwa na Rais anayewajali na kuwathamini walimu na kwamba baada ya kupokea ombi la kuwapandisha madaraja walimu, Rais hakusita kulitekeleza, licha ya ukweli kuwa hatua hiyo ilisababisha ongezeko katika bajeti ya mishahara.
