Mechi ya Yanga SC dhidi ya Simba SC yaahirishwa

DAR-Kamati ya Usimamizi na Uendesha ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza rasmi kuahirisha mchezo wa Ligi Kuu namba 184 kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC uliyopangwa kuchezwa leo saa 1:15 usiku.

Bodi imefanya maamuzi hayo baada ya kupokea taarifa ya awali ya Ofisa Usalama wa Mchezo ambayo imeanisha matukio kadhaa yaliyopekea Simba SC kushtaki kwa TFF na Bodi ya Ligi kutokana na kushindwa kufanya mazoezi.

Bodi ya Ligi imesema mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusiana na sababu zilizosababisha mchezo huo kutochezwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news