Mradi wa Wash waboresha huduma za afya nchini

DODOMA-Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amesema kuwa Mradi wa WARSH umeleta maboresho makubwa katika upatikanaji wa huduma za afya msingi nchini.
Dkt. Mfaume ametoa kauli hiyo alipotembelea Zahanati ya Kijiji cha Manyata, wilayani Kongwa, wakati wa ziara shirikishi ya usimamizi wa huduma za Afya, Lishe, na Ustawi wa Jamii katika Mkoa wa Dodoma.
"Serikali ilitenga zaidi ya Sh.Bilioni 2.16 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matundu ya vyoo, mifumo ya maji, na vichomea taka," amesema Dkt. Mfaume.

Aidha, ameeleza kuwa ili kuboresha usafi na upatikanaji wa maji katika vituo vya afya, Serikali kupitia fedha za Benki ya Dunia na mapato ya ndani, inatekeleza programu ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini katika mikoa 25.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news