DAR-Mtoto pekee wa Hayati Bibi Titi Mohamed Bi. Halima Mzee akiwa na familia yake wamefika nyumbani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa Masaki Jijini Dar es salaam kutoa pole kufuatia kifo cha Baba mzazi wa Mhe. Mchengerwa.

Alhaj Omary Mchengerwa, alifariki dunia alfajiri ya Jumatatu, Februari 24, 2025 akiwa katika Ibada ya Umrah, Medina.