Mwanahabari aguswa na Falsafa ya 4R za Rais Samia, aja na kitabu cha namna yake

NA GODFREY NNKO

KITABU cha Samia na Falsafa ya Samialojia (4R) za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kinatarajiwa kuzinduliwa Machi 19,2025 ambayo ndiyo siku aliyoapishwa Rais Dkt.Samia.
Hayo yamesemwa leo Machi 2,2025 na mwandishi wa kitabu hicho,Derek K.Murusuri wakati akitoa taarifa za awali za uzinduzi wa kitabu hicho katika Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF Commercial Complex, Sam Nujoma jijini Dar es Salaam.

Bw.Murusuri amewaeleza waandishi wa habari kuwa,kitabu hicho chenye kurasa 470 katika hatua ya awali kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo baadaye kitatafsriwa kwa Kiingereza na Kifaransa.
"Samia Logus au Samia Ology sisi tunaitafsiri kama Wazo la Samia au Neno la Samia au Somo la Samia, ndio maana tumepata neno Samialojia."

Amesema, neno hilo limejengwa katika misingi saba ya Reconciliation (Maridhiano),Resilience (Ustahimilivu), Reform (Mageuzi) na Rebuilding (Kujenga Upya).

"Mimi pamoja na wadau wengine mbalimbali wanaoamini, very strongly katika Falsafa angavu ya 4R wameonesha support... unwavering support katika kuhakikisha kazi hii inafikia hatua ya mwisho, ninawashukuru sana, wameweka historia katika kizazi hiki."

Pia, amesema kitabu hicho ni zawadi kutoka kwa wananchi wa kawaida walioona, wakaguswa na utendaji wa Rais katika kuliongoza Taifa na kuwathamini watu.
"Tunaguswa na utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ndiyo maana tukaamua kuandika kitabu, si tu kwa kumpa moyo yeye, bali pia kwa kuhifadhi historia ya mambo mazuri yasije yakachukuliwa na upepo."

Aidha, amesema wanatarajia kueleza ushiriki wa wadau mbalimbali siku ya uzinduzi huku akiweka wazi kuwa, wapo watu wengi wenye mapenzi mema na wanashawishika na uongozi wa Rais Dkt.Samia kupitia Falsafa yake angavu ya 4R. "Sisi tumeivalisha uhusika, Samialojia.

"Kitabu hiki kimeandika mambo mengi katika dhana ya uongozi,nguvu ya kiongozi mwanamke, falsafa angavu ya 4R ya Dkt.Samia Suluhu Hassan, kimeangalia dhana, utekelezaji wake na mafanikio ya utekelezaji wa falsafa hiyo.

"Yaani, falsafa hii imejaribiwa Tanzania kama laboratory na imeonekana kuleta mafanikio makubwa sana katika kujenga amani na utulivu."
Bw.Murusuri amesema kuwa, mafanikio yake sssa yanaweza kuigwa na mataifa mengine mbalimbali si tu barani Afrika, bali pia na duniani kote.

Amesema, kitabu kinatoa mapendekezo maalum na mambo mengine muhimu yanayoweza kuwatia moyo na kuwafunda vijana wa kike na kiume.
"Wanatamani kuwa viongozi bora kupitia nyanyo za Dkt.Samia Suluhu Hassan na kuavha urithi katika kila hatua ya maisha yao."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news