DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amezungumzia kuridhishwa kwake na maboresho ya Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililoko Kivukoni jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo wakati akizungumza na Kamati ya Wataalamu ya Menejimenti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliokutana tarehe 5 Machi, 2025 katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kivukoni jijini Dar es Salaam.

“Ni Matarajio yangu kuwa Ofisi hii ibadilike kutoka kuwa Ofisi ya Mkoa na iwe Sub-head Office,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa upande wake, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno alimshukuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Ofisi hizo, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuzitunza ili ziendelee kuwa bora wakati wote.
