Mwenyekiti wa CHADEMA aibua mapya ya Maria Sarungi na Mdude

SIMIYU-Siku chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuitisha kikao maalum kwa wanachama waliowania ubunge mwaka 2020 na wale wanaopanga kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025,Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Meatu, Francis Kishabi ameibua mapya ndani ya chama hicho.

Kikao hicho kitafanyika Aprili 3,2025 katika Ofisi Kuu za chama, Mikocheni jijini Dar es Salaam, kuanzia saa nne asubuhi.




Kupitia andiko la Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Meatu, Kishabi leo Machi 27,2025 ameeleza kuwa;

Maria Sarungi anaomba majina ya wabunge hao.Swali,kwani Maria ana cheo gani CHADEMA?.

Je, Maria ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa kiasi cha kuagiza apewe majina ya wabunge wa chadema?.

MDUDE

Huyu anasema iwapo chadema itashiriki uchaguzi,yeye Mdude na wenzake watakaa kando na kuwa mwanaharakati huru.

Swali, Mdude ni nani Chadema mpaka atishie chama?.

Hoja ya ujumla kwa wanaharakati Maria na Mdude,Chadema iongozwe kwa katiba na vikao vya chama au kwa misimamo ya wanaharakati?.

Wanapata wapi nguvu ya kutishia,na kutaka kukitishia chama?Nani yupo nyuma ya hawa wanaharakati?.

Chadema ikiwafuata hawa watu, je itakuwa katika misingi yake kama chama cha kisiasa au itakuwa imeacha misingi hiyo?.

Wanaharakati ili wawe tishio kwa serikali hujiambatanisha na vyama vya upinzani. Inaweza kuwa nia nzuri au mbaya.

Wakithibitisha kuwa na sauti ndani ya chama hicho, ndipo huanza NDOA watawala na biashara ya migogoro huanzia hapo.

Mdude na Maria tutawaaminije wao kama hawana UTAPERI juu ya misimamo yao kwa Chadema?.

Tushirikiane kwa tahadhari.

Ishi kwa akiri chadema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news