DODOMA-Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa jengo jipya la Makao Makuu ya TBC Dodoma litasheheni mambo mengi ikiwemo makumbusho ya utamaduni ambapo mzee Moris Nyunyusa na ngoma zake 10 ni miongoni mwa vivutio kwenye jengo hilo.
Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo Jumatano, Machi 12, 2025 wakati alipotembelea jengo hilo linalojengwa Vikonje, jijini Dodoma na kamati ya kudumu ya Bunge ya Habari, elimu, Utamaduni na Michezo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko.
Hayati mzee Nyunyusa ni mlemavu wa macho ambaye alivuma kwa umahiri wake wa kupiga ngoma 17 ambapo moja ya mdundo wake ulitumiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na redio Tanzania kuashiria kuanza kwa taarifa ya habari.