ROATAN-ndege ya LANHSA Jetstream 31 imetumbukia baharini dakika tisa ilipokuwa inapaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Juan Manuel Galvez huko Roatán, Honduras.
Aidha,ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 17 huku abiria wakiwa 14 na wafanyakazi watatu wa ndege, kati yao 12 wamefariki.
Roatan Wilmer Guerrero ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Zima Moto nchini Honduras amethibitisha ajali hiyo ingawa chanzo cha ajali bado hakijafahamika.
Miongoni mwa waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na mwanamuziki maarufu nchini Honduras,Aurelio Martinez Suazo.