DAR-Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) linatarajia kuanza safari za ndege zake kutoka Tanzania kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuanzia Aprili 25,2025.
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii ya ATCL safari hizo za Kinshasa zitakuwa kwa wiki mara nne ikiwemo siku ya Jumatatu, Jumatano,Ijumaa na Jumapili.