Ni wajibu kuandaa jamii yenye maadili na hofu ya Mungu-Rais Dkt.Mwinyi

DAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, ni wajibu kuandaa jamii yenye maadili na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati wa fainali za Mashindano ya 24 ya Kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aisha Sururu Foundation katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Machi 9, 2025.

Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, kazi kubwa imefanyika kuwaandaa vijana kuwafundisha kukihifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran).
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Taasisi ya Aisha Sururu Foundation cha mafunzo ya Quraan na ufundi stadi katika eneo la Kiparan'ganda Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Aisha Sururu Foundation kwa kuendelea kuyaandaa mashindano ya kuhifadhi Quran hadi ngazi ya Taifa kwa kushirikisha washiriki kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Vilevile kwa kuweka mazingatio maalum ya kuwasaidia wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupitia taasisi hiyo.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ametumia fursa hiyo kuziomba taasisi mbalimbali na watu wenye uwezo kusaidia kufanikisha shughuli za kidini ikiwemo za kuhifadhi Quraan ili kuzidi kuuimarisha Uislamu na kupata fadhila nyingi kwa Mwenyezi Mungu.

Washindi mbalimbali wa mashindano hayo ya kuhifadhi juzuu 3, 5, 10, 20 na 30 wamepatiwa zawadi za fedha taslimu.

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post