DAR-Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Joyce Mbaga maarufu kwa jina la Nicole Joyberry kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu na kufanya biashara ya kuanzisha ma-group na kukusanya pesa kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 5, 202 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro imeeleza kuwa matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wakati mwingine nje ya mkoa wa Dar es Salaamn.
“Matukio haya yametokea ndani na nje ya Dar es Salaam, kwa kuhamasisha baadhi ya watu akianzisha ma-group mbalimbali na kuweka majina hewa kwenye ma-group hayo.
"Kwamba wanachangia pesa na baada ya muda mfupi basi utapata kiwango kikubwa cha pesa, jambo ambalo baadaye anakuja kutopatikana kwenye simu na kupotea na pesa ambazo watu wamechangia,”amebainisha Kamanda Muliro.