NIRC yashiriki ziara Kamati ya Bunge jijini Arusha

ARUSHA-Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeshiriki ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kutembelea mradi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika shamba la mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) lililopo Ngaramtoni, eneo lililowekewa miundombinu ya Umwagiliaji Hekta 160 kati ya 200 sawa na asilimia 82 ya utekelezaji, na shamba la Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika kituo cha TARI kilichopo Seliani mkoani Arusha.
Katika utekelezaji mradi huo Tume imeshiriki Kama mshauri mwelekezi katika usimamizi wa mradi.
Aidha, kamati hiyo imeipongeza Wizara ya Kilimo kwa kuwa wabunifu na mipango madhubuti ya kuhakikisha inakabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwekeza katika sekta ya Umwagiliaji na kuongeza Uzalishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news