Ofisi ya Msajili wa Hazina kufanya Mkutano na Kampuni ambazo Serikali ina Hisa Chache

DAR-Ofisi ya Msajili wa Hazina inatarajia kufanya mkutano na wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache, takribani 150 kutoka kampuni 56, kuanzia Machi 25-28, 2025.
Kaulimbiu ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia Machi 25 hadi Machi 28, 2025 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha, Pwani ni ‘Matumizi ya Teknolojia katika Kuboresha Utendaji'.

Mkutano huu unalenga kutoa nafasi ya majadiliano kuhusu mchango wa teknolojia linapokuja suala la maamuzi yatokanayo na data “data-driven decision making” na ufanisi wa taasisi.

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji,Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news