NA VERONICA MWAFISI
OFISI ya Rais-UTUMISHI katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2025 inatoa huduma za Kiutumishi katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume kuanzia tarehe 01 hadi 8 Machi, 2025 jijini Arusha.
Watumishi wa Umma na Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea Banda la Ofisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kiutumishi.
Huduma zinazotolewa katika Banda hilo ni Mifumo ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini ikiwemo e-Watumishi (HCMIS), e-Msawazo (HR-Assessment), e-Uhamisho (Watumishi Portal), e-Mikopo, e-Utendaji, e-Likizo pamoja na e-Mrejesho.
Vilevile katika banda hilo zinapatikana Huduma za Kisheria katika Utumishi wa Umma na hitimisho la kazi kwa kwa Mtumishi wa Umma pamoja na Huduma za Ujumuishwaji wa Anuai za Jamii Mahali Pa Kazi katika Utumishi wa Umma.