ARUSHA-Wanawake watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Machi 8,2025 kitaifa mkoani Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yameongozwa na kaulimbiu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”