Omolo aendesha kikao cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa mwaka 2025/26

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo amefungua Kikao Kazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kinachoshirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage jijini Dodoma.
Kikao kazi hicho kimelenga kufanya uchambuzi wa bajeti ili kuwa na uelewa wa pamoja wa jinsi mipango na rasilimali fedha zinavyoelekezezwa katika afua/maeneo ya kimkakati ili kuwezesha Serikali kufikia malengo ya muda mfupi, wa kati na mrefu kama ilivyoainishwa katika Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2025/26, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP III) pamoja na Sera na vipaumbele vya Kisekta.
Aidha, uchambuzi unalenga kuongeza ushirikiano (synergies) katika utekelezaji wa mipango kati ya Sekta zinazotegemeana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news