DODOMA-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetuma salamu za pole kwa klabu ya Pamba Jiji FC kufuatia ajali ya basi lao iliyotokea Bahi mkoani Dodoma leo saa 11:00 alfajiri.
Wachezaji wa timu hiyo walikuwa safarini kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB, Machi 11, 2025 dhidi ya Kiluvya United.
"Tunawatakia nafuu ya mapema wote waliopata maumivu na Mungu awasimamie katika safari yao. Amin!."