Prof.Janabi miongoni mwa wagombea watano Mkurugenzi Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika

NEW YORK-Shitika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kupokea majina ya wagombea watano (5) wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kwa Kanda ya Afrika akiwemo pia Prof. Mohamed Janabi ambaye anaiwakilisha Tanzania.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya WHO Machi 14, 2025 inaeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Duniani Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amepokea majina ya wagombea hao kutoka nchi wanachama wa WHO Kanda ya Afrika.

Prof. Janabi atachuana na Dkt N’da Konan Michel Yao kutoka Côte d’Ivoire, Dkt. Dramé Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger pamoja na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo.

WHO itaendesha tena uchaguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika hivi karibuni, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika hilo Dkt. Faustine Ndungulile kilichotokea Novemba 27, 2024.

Dkt.Ndugulile aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Pia alikuwa Naibu Waziri wa Afya kati ya mwaka 2017-2020 na Waziri wa Habari na Mawasiliano hadi 2021.

Alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Afrika wa WHO mwezi Agosti na alitarajiwa kuanza jukumu lake jipya Februari 2025, kufuatia Dkt.Matshidiso Moeti ambaye alihudumu katika jukumu hilo kwa mihula miwili.

Katika hotuba yake ya kukubali uteuzi, Dkt.Ndugulile alieleza dhamira thabiti ya kuendeleza afya na ustawi wa watu barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news