ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametoa rai ya kuyafanya Mashindano ya Kuhifadhi Quran Afrika kuwa ya ngazi ya Kidunia.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai hiyo alipozungumza katika Mashindano ya Kuhifadhi Quran Afrika yaliofanyika Uwanja wa New Amani Complex, Wilaya ya Mjini.

Ameeleza kuwa,mafanikio yaliopatikana katika miaka miwili ya mashindano hayo hapa Zanzibar yana kila sababu ya kuyapandisha ngazi na kuwa ya Kidunia.
Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amesema Mashindano ya Kuhifadhi Quraan Afrika ni tukio lingine muhimu la kuutangaza Utalii wa Zanzibar Kimataifa kupitia matamasha na matukio ya aina hiyo pamoja na kuimarisha ushirikiano wa nchi za Afrika na kutekeleza masuala ya kidini kwa pamoja.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Umahiri wa Kuhifadhi Quraan unaooneshwa na Vijana ni Urithi Muhimu kwa vizazi vya sasa na baadae na kusifu Juhudi za Walimu wa Madrasa na kuahidi kwa Serikali kuunga Mkono Mashindano hayo.