Rais Dkt.Mwinyi afuturisha Mkoa wa Kaskazini Unguja,akabidhi sadaka kwa wenye mahitaji maalum

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kuwa wana wajibu wa kufahamu kuwa ni wadau muhimu wa kuhimiza amani kwa ajili ya maendeleo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati akitoa salamu kwa wananchi baada ya kujumuika nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa kwa ajili ya wananchi wa mkoa huo iliofanyika Chuo cha Elimu Mbadala Mkokotoni.
Amewahimiza umuhimu wa kuiombea nchi amani wakati ikielekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba,mwaka huu.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,miaka iliyopita nchi ilikuwa ikiingia katika mifarakano ya kisiasa kila inapoingia katika uchaguzi jambo lisilopaswa kutokea tena hivi sasa.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa,maendeleo yaliopatikana ndani ya miaka minne yamechangiwa na kuwepo kwa amani inayohitaji kudumishwa.
Wakati huohuo Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi Sadaka ya Futari kwa watu wa makundi Maalum wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwemo Wajane, Yatima, Watu wenye Ulemavu na wanaoishi katika mazingira magumu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news