ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi katika makundi maalum wakiwemo wazee, yatima, watu wenye ulemavu,wajane,walimu wa Madrasa, Masheikh na Maimamu wa misikiti wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari ya pamoja aliyoiandaa.
Hafla hiyo imefanyika ZSSF, Tibirinzi Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 18 Machi,2025.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewasisitiza wananchi kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na viongozi wakuu wa nchi.