ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi katika makundi maalum wakiwemo Wazee, Yatima, Watu wenye Ulemavu, Wajane, Walimu wa Madrasa, Masheikh, na Maimamu wa Misikiti wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Futari ya pamoja aliyoiandaa.

Hafla hiyo imefanyika Baraza la Wawakilishi, Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba tarehe 19 Machi 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewasisitiza wananchi kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na viongozi wakuu wa nchi.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi Sadaka ya Futari kwa Watu wa Makundi Maalum wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwemo Wajane, Yatima, Watu wenye Ulemavu, Wazee,Walimu wa Madrasa na Maimamu wa Misikiti.
