ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Futari ya pamoja aliyoiandaa.

Hafla hiyo imefanyika Ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein uliopo Tunguu, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Wakati huo huo Rais Dkt.Mwinyi amekabidhi sadaka ya bidhaa za chakula kwa ajili ya Futari kwa watu wa makundi maalum wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiwemo watu wenye ulemavu,wajane,yatima,watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu.
Rais Dkt.Mwinyi tayari amekabidhi sadaka ya aina hiyo kwa wananchi wa mikoa ya Kaskazini Unguja na Mjini Magharibi.