ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ameipongeza Benki ya Stanbic kwa kuwa mshirika wa maendeleo Zanzibar na kwa kuleta suluhisho za kifedha zenye manufaa kwa nchi na wananchi wa Zanzibar katika miradi ya kimkakati.
Rais Dkt.amesema hayo alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Manzi Rwegasira, Ikulu Zanzibar mapema leo.

Ameeleza kuwa Benki ya Stanbic, kufuatia utiliaji wa saini wa mkataba wa leo kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), tayari itakuwa zimeshatoa jumla ya mkopo wa pamoja shilingi bilioni 185 kati ya bilioni 500 zinazohitajika kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kufadhili miradi ya maendeleo.