ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza wananchi kuendelea kuiombea nchi amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na viongozi wakuu wa nchi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi 18,2025 wakati akikabidhi Sadaka ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ya bidhaa za chakula kwa ajili ya futari kwa watu wa makundi maalum wa Mkoa wa Kusini Pemba wakiwemo watu wenye ulemavu, wajane, yatima, wazee, walimu wa Madrasa na Maimamu.