ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekabidhi Sadaka ya Futari kwa wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Makabidhiano hayo yamefanyika Viwanja vya Mapinduzi Square huko Michenzani ambapo wananchi mbalimbali waliojitokeza kupokea sadaka hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa,sadaka hiyo imetolewa na mfadhili ndugu Jaffar aliyemkabidhi Dkt.Mwinyi ili kuwagawia wananchi.
Rais amemshukuru hfadhili huyo na wananchi waliojitokeza kuipokea.
Wakati huohuo Rais Dkt.Mwinyi amekabidhi sadaka hiyo ya bidhaa za chakula kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mjini Magharibi ili kuendelea na ugawaji kwa wananchi katika wilaya wanazoziongoza.