ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Machi 14,2025 amemteua ndugu Kombo Hassan Juma kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Zanzibar.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,Mhandisi Zena Ahmed Said.