Rais Dkt.Mwinyi awashukuru wadau mbalimbali wanaojitolea sadaka kwa wananchi mbalimbali
ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kujitolea sadaka kwa watu wenye mahitaji maalum katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokabidhi sadaka mbalimbali zilizotolewa na mfanyabiashara Said Nassir Nassor (Bopar) kwa wananchi wa Chanjamjawiri Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 19 Machi 2025.