ZANZIBAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kuwapangia vituo mabalozi.

i.Bi. Rachel Stephen Kasanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi. Bi.Kasanda anachukua nafasi ya Bw. Lauteri John Kanoni ambaye uteuzi wakeumetenguliwa;
ii.Prof. Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi yaWadhamini ya Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania;
iii.CPA.Ashraph Yusuph Abdulkarim ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo
;iv.Balozi Hamad Khamis Hamad amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji;na
V.Balozi Mobhare Holmes Matinyi amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.