Rais Dkt.Samia atoa maagizo Mamlaka za Serikali za Mitaa

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa serikali za mitaa kote nchini kujiepusha kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao, akiwataka kuwa sehemu ya masuluhisho ya migogoro hiyo.
Wakati wa Mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Alat katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma leo Machi 11, 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo ameitaja migogoro ya ardhi kama donda sugu kwenye jamii, akiitaja kama chanzo cha uhasa na mauaji kwenye ngazi ya jamii.
Katika hatua nyingine Rais Samia amewataka watendaji wa Serikali za mitaa kuendelea kusimamia watumishi na watendaji wa mamlaka zao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuwapokea na kuwasikiliza kwa busara sambamba na kuimarisha mifumo ya ushughulikiaji wa kero za wananchi kwa wakati.
Rais Samia pia katika hotuba yake amesisitiza kuhusu kuainisha mipango ya ngazi ya Halmashauri na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na kusisitiza juhudi zaidi katika kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato na kujiepusha na migogoro kati yao na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali na badala yake wakuze na kuimarisha mahusiano mazuri kati yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news