Rais Dkt.Samia atunukiwa tuzo mbili za mwana mageuzi Sekta ya Maji barani Afrika

DAR- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo mbili za kuwa mwana mageuzi katika Sekta ya Maji ndani na nje ya Tanzania.
Miongoni mwa tuzo alizotunukiwa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ni ya Mageuzi katika Sekta ya Maji (THE WATER GAME CHANGER).

Tuzo hiyo imetolewa na Wizara ya Maji ikithibitisha mageuzi katika Sekta ya Maji.
Aidha, tuzo hii inaonesha maendeleo katika Sekta ya Maji na inaunga mkono utekelezaji wa Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.

Tuzo ya pili, Mheshimiwa Rais ametunukiwa ya Kinara wa Masuala ya Maji Afrika (THE PANAFRICAN WATER, SANITATION AND HYGIENE CHAMIPION AWARD).

Hii ni tuzo ambayo imetolewa na Taasisi ya WaterAid UK ya nchini Uingereza.

Kupitia tuzo hii, Mheshimiwa Rais anateuliwa kuwa mlezi wa masuala ya Maji barani Afrika (PanAfrica Water Champion).
Vilevile, tuzo hii inampa hadhi ya kumtua ndoo kichwani Mama wa Afrika na inaongeza sauti ya maji katika ngazi za Wakuu wa Nchi na Serikali wa Bara la Afrika.

Aidha, inatambua mchango wa Mheshimiwa Rais kwenye Sekta ya Maji Kimataifa na inaimarisha ushirikiano wa Kimataifa katika Sekta ya Maji.

Kuanzia leo,Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mlezi wa masuala ya Maji,Usafi wa Mazingira Afrika (PanAfrican Water and SanitationChampion).

Hii ni Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani ambayo inavuka Mipaka yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news