Serikali itaendelea kushirikiana na Vodacom Tanzania-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Vodacom Tanzania katika kuharakisha huduma za kidigitali nchini.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Machi 1,2025 alipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire na ujumbe wake Ikulu Zanzibar.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire ameeleza kuwa Vodacom itapanua huduma zake Zanzibar kwa ajili ya uwekaji wa huduma za kidigitali katika sekta muhimu ikiwemo elimu, afya, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Halikadhalika, Besiimire amesema Vodacom Tanzania kupitia Foundation yake itajitolea kuboresha zaidi miundombinu ya kujifunza kielektroniki na kuwawezesha vijana na wanawake kwa ujuzi wa kidijitali na kifedha ikiwemo pia kuunganisha zaidi ya shule 100 Zanzibar ifikapo 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news