NA LWAGA MWAMBANDE
MACHI 4,2025 katika kongamano la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alielezea jinsi watu wanavyotafsiri kukatika kwa umeme kama kosa la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) bila kujua sababu halisi.
Picha na CRO.
Kupitia kongamano hilo ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Dkt.Biteko alikumbuka tukio aliloshuhudia wakati akiwa kanisani ambapo umeme ulipokatika, waumini walimgeukia kwa kuwa yeye ni waziri mwenye dhamana ya nishati na wakiamini ni changamoto ya huduma kutoka TANESCO.
Aidha, Naibu Waziri Mkuu alipouliza sababu ya kukatika kwa umeme kumbe ilikuwa Luku imeisha. Baada ya ujumbe huo, mshairi wa kisasa,Lwaga Mwambande anabainisha haya. Endelea;
Mwingine unakatika, luku kwisha si TANESCO,
Hivyo mkilalamika, si kila kitu TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
2. Kasema kisa kimoja, kanisani akiweko,
Kukatika mara moja, wote macho kwa Biteko,
Mioyoni yao hoja, kwamba hiyo ni TANESCO
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
3. Dhamana yake nishati, yuko juu ya TANESCO,
Ndivyo walivyomseti, kwamba ahoji TANESCO,
Kumbe sababu si nyeti, ya kuikaba TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
4. Aliulizauliza, na sababu ikaweko,
Luku walivyoijaza, yuniti kumbe haziko,
Hapo bure twaikwaza, kudai kwamba TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
5. Umeme unakatika, si mara zote TANESCO,
Wao kama wakatika, hutuambia TANESCO,
Kama kazi yafanyika, na usalama uweko,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
6. Luku ulivyonunua, ikiisha si TANESCO,
Kimbia nenda nunua, umeme utakuweko,
Hapo nawe utajua, ni wewe siyo TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
7. Mashine nyingi za LUKU, walizoleta TANESCO,
Umeme kama kiduku, tahadhari yao iko,
Sikiza kelele kuku, usilaumu TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
8. Pengine ni nyaya mbovu, unalaumu TANESCO,
Kutengeneza mvivu, kelele ni kwa TANESCO,
Uache huo uchovu, uifaidi TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
9. Mnafanya kazi nzuri, hongera kwenu TANESCO,
Umeme wenu mzuri, kwa wengi una mashiko,
Na tena hamsubiri, mnapoitwa TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
10. Kama ni matengenezo, mnatwambia TANESCO,
Hakuwi na matatizo, kulalamika TANESCO,
Hapo mwandoa kwazo, tuhudumie TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
11. Nishati hii umeme, nchi yetu ni TANESCO.
Mema yao tuwaseme, wayafanyayo TANESCO,
Na kukosoa tuseme, wawe vizuri TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
12. Sante Dokta Biteko, ujumbe una mashiko,
Endapo lawama ziko, siyo zote za TANESCO,
Kuwajibika kuweko, si lawama kwa TANESCO,
Ni kiongozi mkubwa, ambaye atukumbusha.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602
Cha ajabu ukiwaka, hatajwi tena Biteko,
ReplyDeleteLakini ukikatika, anadhulimiwa heko,
Kebehi na hekaheka, uzushi na chokochoko,
Hili shirika TANESCO, linastahili heko.
Majuzi ulikatika, ikazuka sokomoko,
Sauti ikisikika, "huku tuendako siko,
Fujo na manung"uniko, yowe na malalamiko,
Lisipewe TANESCO, kongole tutoe heko.