Simba SC yatinga 16 bora CRDB Federation Cup

DAR-Kikosi cha Simba SC kimetinga hatua ya 16 bora ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TMA Stars katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Kupitia mchezo huo wa Machi 11,2025 mlinzi wa kushoto, Valentine Nouma aliwapatia bao la kwanza dakika ya 17 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya Awesu Awesu Awesu kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Dakika mbili baadae Sixtus Sabilo alijifunga na kuwapatia Simba SC bao la pili katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.

Aidha,kipindi cha pili walirudi kwa kasi ya kawaida huku wakimiliki sehemu kubwa ya mchezo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa TMA, lakini walikosa ufanisi wa kutumia nafasi tulizopata.

Leonel Ateba aliwapatia bao la tatu dakika ya 75 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kelvin Kijili.

Ushindi huo unaifanya Simba SC kukutana na timu ya Big Man inayoshiriki Championship kutoka Korogwe, Tanga kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora baadae mwezi ujao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news