SINGIDA-Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi kuzindua uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium uliopo katika eneo la Mtipa mkoani Singida.
Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025 mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga SC.
"Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki na jamii kwa ujumla.
"Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.