DAR-Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika jijini Dar es Salaam,SP Awadh Mohamed Chiko unatarajiwa kuzikwa leo Machi 18, 2025 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kukamilika kwa taratibu za kijeshi.
SP Awadh Mohamed Chico amefariki dunia jana majira ya asubuhi kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Pugu Sekondary.
Ni baada ya dereva wa Daladala yenye usajili namba T 580 EAE aina ya TATA inayofanya safari zake kati Zingiziwa Chanika na Machinga Complex Ilala akitokea Pugu kwenda Gongo la Mboto kugongana na gari T 952 AMD aina ya Toyota Prado.
Gari hiyo ilikuwa ikiendeshwa na PF 15950 SP Awadh Mohamed Chico ambaye ni mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika akitokea Gongo la Mboto kuelekea Pugu na kusababisha kifo chake hapohapo.
Aidha,kabla ya kuzikwa, mwili wa marehemu SP Awadh utaswaliwa katika msikiti wa Akachube uliopo Kijitonyama na kwa sasa msiba upo nyumbani kwakwe Kijitonyama Mtaa wa Bukoba.