Steven Mukwala apiga hat trick, Simba SC yailiza Costal Union

ARUSHA-Mshambuliaji Steven Mukwala amefunga hat trick katika ushindi wa mabao 3-0 kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Hat trick hiyo ya Machi 1,2025 ambayo ni ya kwanza kwake msimu huu imemfanya Mukwala kufikisha mabao nane kwenye ligi mpaka sasa.

Mukwala aliwapatia Simba SC bao la kwanza dakika ya 30 kwa shuti kali la chini chini baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta ‘Duchu’.

Aidha,Mukwala aliwapatia bao la pili dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

Mukwala aliwapatia bao la tatu dakika ya 57 baada ya kumalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango Chuma Ramadhani kufuatia shuti kali lililopigwa na Mpanzu.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kufikisha alama 54 baada ya kucheza mechi 21 wakiwa nafasi ya pili huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news