DAR-Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeupangia tarehe mchezo namba 148 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC ya Dar es Salaam na Dodoma Jiji ya mkoani Dodoma, uliokuwa umeondolewa kwenye ratiba ya ligi baada ya Klabu ya Dodoma Jiji kupata ajali ya gari walipokuwa wakisafiri kutoka mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi jioni hii imeeleza kuwa, mchezo huo sasa utachezwa Machi 14, 2025 kuanzia saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa KMC Complex uliopo, Mwenge, Kinondoni, Dar es Salaam.