DODOMA-Tume ya Utumishi wa Umma imepewa mamlaka ya kupokea na kushughulikia Rufaa naMalalamiko ya watumishi wa umma ambao hawajaridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri,Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu katika Utumishi wa Umma.
Hii ni kwamujibu wa Kifungu cha 10(1)(d) na Kifungu cha 25(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa UmmaSura ya 298 [Marejeo ya Mwaka 2019J.
Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1)(c) cha Sheria hiyo, Tume ina wajibu wa kuhakikisha Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka za Nidhamu wanasimamia Utumishi wa Umma kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu naMiongozo ya Utumishi wa Umma.
Hivyo, tarehe 03/03/2025, Tume ya Utumishi wa Umma itaanza Mkutano wake Na. 3 kwaMwaka wa Fedha 2024/2025.
Aidha, kuanzia tarehe 04/03/2025 hadi 06/03/2025, Tume itafanya Ziara ya Kujifunza pamoja na kutoa elimu ya masuala ya Kiutumishi katikaWakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) Jijini Dar es Salaam.
Kuanzia tarehe 10/03/2025 hadi tarehe 21/03/2025, Tume itaendelea na Mkutano wake Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (USCAF) ambapo itajadili na kutoa uamuzi wa Rufaa na Malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka zao za Nidhamu.
Katika Mkutano huo, pia, Tume itatoa nafasi kwa Warufani na Warufaniwa walioombakufika mbele ya Tume kutoa ufafanuzi wa ziada kuhusu hoja zao za Rufaa mbele ya Tume.