Tanzania kushiriki Mkutano wa Mwaka wa PDAC nchini Canada

TANZANIA inatarajia kushirikia mkutano Mkuu wa mwaka 2025 wa jumuiya ya Watafiti na Wawekezaji wa Sekta ya Madini nchini Kanada (PDAC) unaotarajiwa kufanyika jijini Toronto kuanzia Machi 2 hadi 5, 2025.
Katika Mkutano huu, Tanzania itawakilishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) , ambalo litakuwa miongoni mwa washiriki kupitia MineAfrica Inc kwenye maonesho ya PDAC.

STAMICO itakuwa katika banda namba 923 lililo katika jengo la kusini katika kituo cha mikutano cha Metro Toronto.
Ushiriki wa Tanzania kupitia STAMICO katika mkutano huu ni fursa muhimu ya kutangaza na kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini.

Pamoja na mambo mengine, katika mikutano iliyopita STAMICO imekuwa ikinadi na kutangaza fursa za uwekezaji katika madini ya metali hususan dhahabu na madini muhimu kama vile madini ya Lithium,Kinywe, Cobalt, Tina, chuma na madini ya Rare Earth Element (REE) kwa lengo la kuwakaribisha wawekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news