MWANZA-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokudhi vigezo vya kikanuni na Sheria za Mpira wa miguu.
Uwanja huo ulifungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoanishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.
Aidha,TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki (kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja), ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya ligi.