ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wananchi kuendelea kuiombea nchi amani ili maendeleo zaidi yapatikane.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Machi 21,2025 alipojumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Weles Kikwajuni Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amefahamisha kuwa,kipindi cha miaka mitano ya Awamu ya Nane mambo mengi ya maendeleo yamefanyika katika nyanja zote kutokana na nchi kuwa na amani,hivyo kuna wajibu wa kudumishwa.