ARUSHA-Watumishi wanawake wa Tume ya TEHAMA, leo wameungana na wenzao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Arusha. Wakiwa Arusha, watumishi hao walitembelea pia Kiwanda cha vifaa vya TEHAMA cha TanzTech cha jijini Arusha na eneo kinapotarajiwa kuwekwa kituo cha ubunifu wa TEHAMA, SIDO, Arusha.