Tunataka kuwa champion wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050-Mwanasheria Mkuu wa Serikali

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki kikamilifu katika kutoa maoni katika utengenezaji na uandaaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ili kuhakikisha kuwa Dira hiyo inaakisi masuala yote ya Sekta ya Sheria.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amezungumza hayo katika mahojiano maalumu na Vyombo vya Habari yaliyofanyika Ofisini kwake, Mtumba jijini Dodoma, tarehe 10 Machi, 2025.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa Ofisi yake imejipanga kuhakikisha kwamba mambo yote yanayoihusu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanatekelezwa ipasavyo ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050.

“Sisi kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tutahakikisha kwamba tunaoanisha vizuri Sheria zetu tulizonazo na kule tunakotaka kwenda, ni lazima tuwe na legal framework ya kutufikisha,”amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesisitiza suala la kufanya maboresho katika Sheria mbalimbali ziweze kuendana na mabadiliko ya Kijamii, Kiuchumi pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa Sheria.

“Sisi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunataka kuwa champion wa kuhakikisha kuwa sheria zetu zote tunazioanisha na Dira ya Taifa ya 2050,”amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika hatua nyingine Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongelea suala la ufasiri wa Sheria, ambapo amasema kwakua Sheria mbalimbali zimeweza kutasfiriwa kutoka lugha ya Kingereza kwenda Kiswahili kwakuwa ili ziweze kutumika kwa urahisi na watumiaji.

“Kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Desemba 2024 tumeweza kutafsiri jumla ya Sheria kuu 300 lengo kubwa ikiwa ni kuwarahisishia watumiaji wa Sheria,”amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Sambamba na hilo, Mhe. Johari amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeweza kukamilisha zoezi la Urekebu wa Sheria, ambapo Sheria mbalimbali zilizorekebishwa zimeweza kufanyiwa Urekebu, hivyo watumiaji wa Sheria watapata Sheria hizi zikiwa zimerekebishwa kwa wepesi zaidi.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekuwa ikitoa huduma za Ushauri wa Kisheria bila malipo kwa wananchi kupitia Kliniki za Ushauri wa Kisheria kwa kushirikiana na Kamati za Ushauri wa Kisheria zilizoko katika ngazi ya Mikoa na Wilaya.
Mhe. Johari ameeleza kuwa kufanyika kwa Kliniki hizo ni mojawapo yah atua za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kusogeza huduma za Kisheria karibu na Wananchi.

“Lengo kubwa la kliniki hizi ni kusogeza huduma za kisheria karibu na Wananchi, huku tukitimiza yale matakwa3 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa kusogeza huduma kwa wananchi,”amesema Mhe. Johari.

Pia, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa kupitia Kliniki za Kisheria Ofisi yake imeweza kutatua changamoto za Kisheria zinazowakabili wananchi katika mikoa mbalimbali, huyu akiyataja masuala ya Ardhi, Mirathi, Ajira, Unyanyasaji wa Kijinsia kuwa ni masuala yanayojitokeza mara kwa mara wakati wa kuhudumia wananchi kupitia Kliniki hizo.

“Tumeweza kufanya Kliniki hizi katika Mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza ambapo jumla ya Wananchi 1,845 wameweza kupata huduma za Ushauri wa Kisheria bure kutoka kwa timu ya wataalamu wetu,”amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news