KATIKA mjadala wa kisiasa unaoendelea kuhusu uchaguzi wa mwaka 2025, Mbunge wa zamani wa Singida Mashariki na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amejikuta kwenye wakati mgumu aliposhindwa kutetea hoja yake ya "No Reforms, No Elections" (Hakuna Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi).
Lissu, ambaye amekuwa mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, alipata wakati mgumu wakati wa mahojiano na vyombo vya habari alipoulizwa swali la msingi:
"Ikiwa serikali haitafanya mabadiliko mnayoyataka, je, CHADEMA haitashiriki uchaguzi wa 2025?"
Ukwepaji wa Swali na Ukimya wa Lissu
Badala ya kutoa jibu thabiti linaloendana na msimamo wake wa muda mrefu, Lissu alikwepa swali hilo na kuanza kuzungumzia masuala mengine yasiyohusiana moja kwa moja na swali aliloulizwa.
Hatimaye, aliamua kususia swali hilo kwa kukwepa kujibu moja kwa moja kama chama chao kitasusia uchaguzi au la.
Tabia hii ya ukwepaji wa maswali muhimu imeibua mjadala miongoni mwa wachambuzi wa siasa na wanaharakati wa demokrasia.
Wengi wanaona kuwa kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections" ilikuwa zaidi ya mbinu ya kisiasa isiyo na mkakati wa utekelezaji.
Mabadiliko Yaliyo Fanyika na Ukweli wa Siasa
Licha ya madai ya Lissu na CHADEMA kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika, ukweli ni kwamba serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mabadiliko kadhaa katika mifumo ya kisiasa na uchaguzi.
Mfano ni kuruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara bila vikwazo, hatua ambayo imesifiwa hata na viongozi wa upinzani waliokuwa wakilalamikia zuio hilo katika awamu iliyopita.
Swali linalobaki ni:Je, CHADEMA iko tayari kususia uchaguzi wa 2025?
Kama msimamo wa Lissu unavyoonyesha, hakuna uhakika wowote wa kususia. Badala yake, inaonekana kauli mbiu hiyo ni mbinu ya kushinikiza bila dhamira halisi ya utekelezaji.
Kwa hali ilivyo sasa, upinzani unapaswa kutathmini upya mkakati wake na kuwa na msimamo thabiti unaoeleweka kwa wanachama na wafuasi wao badala ya kutumia vitisho visivyotekelezeka vya kususia uchaguzi.
Wakati ukifika, ni wazi kuwa CHADEMA italazimika kushiriki katika uchaguzi, hata bila mabadiliko wanayoyataka, jambo linaloifanya kauli mbiu ya "No Reforms, No Elections" kupoteza maana.
Tags
Habari