Tuwekeze Zanzibar SUKUK kwa maendeleo ya nchi-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezishauri taasisi za fedha na kampuni mbalimbali kuwekeza katika hatifungani ya Zanzibar Sukuk kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo Machi 20,2025 alipozungumza na Watendaji wa taasisi za fedha na kampuni waliofika Ikulu Zanzibar.

Aidha,Rais Dkt.Mwinyi amezihakikishia taasisi hizo kuwa Zanzibar Sukuk ni salama na sahihi kuwekeza na kuwaomba kuunga mkono juhudi za Serikali.
Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuwa na fedha za uhakika za kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Halikadhalika amefahamisha kuwa,Zanzibar Sukuk imeweka kiwango kinachoridhisha cha asilimia 10 .5 cha faida kwa anayewekeza ili wadau wengi zaidi wawekeze.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa,benki zote zinazotoa huduma za Fedha kwa Misingi ya Kiislamu zina fursa ya kuwekeza Zanzibar Sukuk.

Aprili 11, 2025 ndio tarehe ya mwisho ya kuwekeza katika Zanzibar Sukuk.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news