Tuzo za TFF, Prince Dube ndiye mchezaji bora mwezi Februari

DAR-Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Prince Mpumelelelo Dube amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC 2924/25 akiwashinda Stephanie Aziz Ki pia wa Yanga Sc na Selemani Bwenzi wa KenGold Fc.
Pia, kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kocha wa Yanga Sc, Miloud Hamdi ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari akiwashinda Fadlu Davids na Fred Felix Minziro.

Dube alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo saba, Yanga SC ikishinda mechi sita na kutoka sare mchezo mmoja akifunga magoli matano na kuhusika kwenye magoli mengine matano.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news